Image result for milki yako 

Kila binadamu amejaliwa vitu vifuatavyo,,::::
1. Ubongo
2.Vipaji/ talanta
3.Muda
4.Ndoto.
5. Maarifa yatokanayo na Elimu dunia.
Vitu hvi vitano vinafanya kazi kwa kushirikiana. pale kimoja kinaposhindwa kufanya Kazi vizuri basi name kingine kinakwama. Japokuwa kuna baadhi ya vitu ni POWERFUL kuzidi vingine. Ngoja tupitie kimoja baada ya kingine
1.UBONGO/BRAIN
Kila kiumbe hai kina ubongo. Ubongo umegawanyika ktk sehemu kuu tatu: ubongo wa mbele, wa kati na wanyuma. Ubongo wa mbele ndio mkubwa na hufanya kazi zifuatazo::::
1.Una tuongoza katika kufikiri, kureason, kujifunza, kutunza kumbukumbu, kufanya maamuzi, kudisplay tabia zetu, kutoa SPEECH, kuona na hutuongoza ktk kutambua kipi tunachokipenda na kipi tunachokichukia.
Sasa  fikiri,, Je wewe ubongo wako wa Mbele unatofauti na wa wengine? Si unafikiri, si unatoa maamuzi, si unauwezo wa kureason?, si unauwezo wa kujifunza na kutunza kumbukumbu? Sasa  inakuwaje mtu anakalia kulaumu ooh me sina BAHATI, mara hawa walijaaliwa na maneno maneno kibao hadi ya kumkufuru Mungu.
UTAJIRI wa kwanza mungu aliotupa sisi wanadamu ni AKILI. Akili iko ndani ya ubongo. Akili hutufanya kujitambua na kujua mema na mabaya. Sasa  tujiulize hv kweli akili zetu tunazitumia???
Bila akili mtu asingejua kuwa ardhini kuna dhahabu au almasi. Bila akili mtu asingejua dhamani ya miliki zote zilizo katika maji na katka miamba. Shida ni kwamba hatujua kuwa akili ni INACTIVE If not IN USE. But the more you use your brain, it becomes stronger and stronger in performing its functions. Tutambue kwamba kitu chochote kikitunzwa tu bila kutumika hufifia na mwishoe kupoteza dhamani yake.
2. VIPAJI/ TALANTA.
Kila mtu pia amejaaliwa kipaji/ vipaji flani japo si kila mtu anatambua kipaji/vipaji vyake. Ndugu yangu nataka nikwambie leo watu ambao ni MA STAR duniani wametambua vipaji vyao na wanavipa kipaumbele ili kuwafikisha mahali wanapotaka kufika.
Mfano angalia kama wasanii Wa musiki, filamu.. Hawa watu tunawasifiaga kwa kufanya vizuri na wanapokuwa wanapresent Kazi zao watu kupata hisia za kazi zao nzuri hadi kudiriki kusimama na kwenda kuwatuza majukwaani.
Wana michezo mbali mbali kama vile mpira na riadha. Hawa ni watu wanaopata umaarufu kwa kutumia vipaji vyao kwa ukamirifu na huwafanya waishi vizuri Maisha yao yote. Mchezaji hata akiwa hachez labda ana maumivu bado Pesa yake inaflow tu. Pia watu hawa hugombaniwa na timu kubwa kubwa kununuliwa kwa gharama zozote zle.
Mtu kama diamond akitoa wimbo mmoja ndani ya mwaka atakula tu na kuishi Maisha ya tofauti sana
Lakini swali linabaki kuwa moja. Je sisi wengine tunaoganga ganga njaa hatuna talanta? Ama kama umejua kama una talanta unaitumia au umeiacha tu ife? Tafakari na chukua hatua
3.MUDA.
Muda ni rasirimali nyingine kubwa sana tuliyojaaliwa kuwa nayo hapa duniani.
Binadamu wote tuna muda wa siku, au miezi  unaolingana. Kuna masaa 24 ktk siku Moja na siku 30/31 ndani ya mwezi mmoja.
Watu wasikini wengi hulaumu laumu kuwa wanakosa muda wa kufanya vitu ABC. LAKINI MATAJIRI huwezi ukawasikia wanatoa excuse ya muda hata siku moja. Wanajitahidi kuu exhaust muda walio nao to the maximum.
Hupangilia shughuli zao za kukamilisha ktk siku husika. Huenda na muda na hawatoi promise fake za kwamba nitafika saa NNE harafu afike SAA nane.  Matajiri na watu wote wanaotafuta Pesa kwa uchungu huamka mapema SAA 10/11 alfajiri na hulala wamechelewa approximately saa 5/6/7 usiku. Masikini sisi kwanza kukilala tumechelewa labda tulikuwa vilabuni, kwenye sherehe au tulikuwa tunatizama movies mbalimbali.
Siku zote tutambue kuwa kama tukifanya kazi bila ratiba na bila kujari muda hatutafanikiwa katika  ndoto zetu.  Tujifunze kutumia muda kwa umakini.
Mungu alijua kuwa 24 hours yanatosha kwa shughuli zetu za siku. Tusimkufuru Mungu kwa lawama zisizo za msingi.
Kila siku jipangie Kazi za kukamilisha na utashangaa jinsi mambo yako yatakavyoenda vizuri
4. NDOTO/DREAMS
Kila mtu ana ndoto moyoni mwake ya kutimiza kabla hajatoweka duniani
Ndoto yako ni lile wazo lako juu ya kukamilisha jambo Fulani. Baadhi ya watu ideas/ dreams zao ni kuwa viongozi, wakulima, wafugaji, wafanya biashara wakubwa ama kuwa wasanii wakubwa. Kumiliki majumba, magari na kusomesha watoto wao ktk Shule za hadhi.
Kila idea/ dream ni nzuri kulingana na mtu mwenyewe anayeimiliki hiyo ndoto.
Lakini research nyingi zinasema, aslimia 98% ya watu wanaokufa wanakufa na ndoto zao. Na asilimia Moja(1%) wanakufa wakiwa kwenye msingi wa kuanza kutimiza ndoto zao na only 1% wanakufa wametimiza ndoto zao
Wapendwa vle ujiwaziavyo ndivyo ulivyo. Kama unawaza kuwa kwa nguvu zako unaweza kufanya vitu fulani huo ni ukweli unaweza. Na vlevle kama unawaza kuwa hauwezi kufanya vitu fulani ni kweli huwezi.
Katika maongezi yangu huwa napenda kuzungumzia challenges za Maisha na namna ya kujikwamua ktk challenge hzo. Lakini ninachokigundua ni kuwa hakuna mtu asiye na mipango. Isipokuwa tu ni kwamba watu wanajipa moyo kuanza baadae eti wakisha SETTLE. Unamshirikisha mtu vtu vya kumsaidia haraka harafu anakwambia eti bado sijasettle maybe mpaka mwakani. Mwakani kukifika mtu anamatatizo zaidi ya mwaka Jana.
Kwa hvo wapendwa nawashauri, unapoanza kuwaza kufanya jambo Fulani litakalo kutoa level uliyopa hadi nyingine, anza Mara Moja maana ukisubiri sana utakwamishwa na vitu ama watu wanaoitwa DREAM KILLERS. Mara tu ukibambana na dream killer sahau kutimiza ndoto zako mapema
5. MAARIFA YATOKANAYO NA ELIMU DUNIA.
Namshukuru mungu kuniwezesha kupata Elimu dunia ya  darasani na ya nje ya darasa. Elimu hii inazidi kunifambua macho yangu ya  ndani ya ubongo  na macho ya nje kwa kunionesha fursa kibao zinazonizunguka.
Maarifa tuliyonayo wasomi ni mengi. Anza kukumbuka somo la stadi za kazi tulizofundishwa Shule ya msingi. Kuna watu leo wamejiajiri wana saloon za kike. Wanasuka nywele mitindo yote. Kuna watu wanatengeneza majanvi, vikapu, ni wachiraji nk lakini haya ni maarifa waliyojifunza ndani na nje ya darasa. Leo mtu anafikiria eti mpaka apate degree, masters au PhD ndo atapata Pesa za kumtoshereza. Hivi umewahi kukaa na wasomi wengi ukawasikia views zao? Tujianzie sisi wenyewe, ni aibu
Ni aibu kushindwa ku apply maarifa tuliyoyapa shuleni na katka mazingira kutufanya matajiri. Matajiri waliowengi si wasomi sana bali ni wabunifu sana.
Hutumia elimu kidogo waliyonayo na maarifa ya Maisha ya binadamu ya kila siku kujitengenezea msingi mzuri wa kujiinua kiuchumi. Hivyo basi ni vema tutumie maarifa tuliyonayo kulingana na standard ya Elimu tulizojaaliwa kuwa nazo kujiingizia kipato.

No comments

Powered by Blogger.